Mgogoro wa fedha Yanga ulivyopelekea kuzaliwa Simba SC

0
101

Historia ya kuanzishwa kwa Young Africans inarudi nyuma hadi miaka 1910, lakini historia ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC ilianza zaidi ya miaka 20 baadaye, miaka ya 1935.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930, Yanga, wakati huo ikifahamika kama New Young iliishiriki Ligi Daraja la Pili Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuapanda ngazi hiyo, na waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Mwaka 1935 uwezo wa klabu ulishuka sana kusababisha wanachama kutofautiana na kuleta migogoro katika klabu na kupelekea baadhi ya wanachama kujiengua na kuanzisha Klabu nyingine.

Wanachama walioasi waliunda Klabu iliyojulikana kwa jina la Queens F.C. ambayo baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Sunderland ambayo kwa sasa inajuliakana kama Simba S.C.

Baada ya mgawanyiko wanachama waliobaki waliifanyia marekebisho klabu yaliyopelekea kubadilisha jina kutoka New Youngs to Young Africans. Mashabiki wengi walishindwa kutamka jina la Young kwa ufasaha ambao ilipelekea kuzaliwa kwa jina la “Yanga”.

Tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania, Simba imetwaa kombe hilo mara 22, huku mahasimu wao Yanga akilibeba mara 27. Hata hivyo, kwa ujumla, Simba ndio timu yenye makombe mengi Tanzania tangu mwaka 1965 ikivuna jumla ya makombe 54.

Unaweza kudhani Simba kutwaa ubingwa mara nne mfululizo tangu 2017 hadi 2021 ndio rekodi yao kubwa zaidi, lakini wamewahi kutwaa kombe hilo mara tano mfululizo tangu mwaka 1976 hadi 1980.

Pia Simba imenyakua Kombe la Nyerere ambalo sasa hivi halipo, walilolitwaa mara tatu mwaka 1984, 1985 na 2000, na mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 2002 amabapo JKT Ruvu walilitwaa kombe mbele ya KMKM.

Kombe la Muungano imeshinda mara tano mwaka 1993, 1994, 1995, 2001, na 2002 na kombe la Mapinduzi ambalo Simba amelitwaa mara tatu mwaka 2008, 2011 na 2015.

Ubingwa wa Tusker umelibeba mara nne mwaka 2001, 2002, 2003 na 2005 na mara moja kombe la Banc ABE Super8 mwaka 2012 na Hedex mwaka 2001.

Mtani Jembe Simba ilichukua mara mbili mwaka 2012 na 2013 wakati kombe la FAT ikibeba mara tatu 1995,2000 na 2017.

Ngao ya Jamii imekwenda Msimbazi mara sita mwaka 2001, 2011, 2012, 2017, 2018 na 2019 huku Kagame nayo ikinyakua mara sita pia mwaka 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002.

Rekodi nyingine tamu kwa simba imewahi kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1974, hatua ya makundi 2003 na robo fainali 2019 wakati fainali ilifika mwaka 1993.

Send this to a friend