Mgombea Ubunge Siha auawa katika ugomvi

0
105

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema linafanya uchunguzi tukio la kuuawa kwa Daud Mtuyehabi, aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Siha.

Tukio la kujichukulia sheria mkononi limetokea Oktoba 7, 2025 majira ya saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Kilingi, baada ya Mtuyehabi kudaiwa kumchoma kisu tumboni Abdul Mohamed, mkazi wa Kilingi, Kata ya Sanya Juu wakati akiamulia ugomvi uliozuka kati ya Mtuyehabi na Hamad Mohamed wakati wakinywa pombe, kutokana na kudaiana fedha.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia Daudi Mtuyehabi hadi kusababisha kifo,” imesema taarifa.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito na kukemea tabia za watu kujichukulia sheria mkononi.

Send this to a friend