Mgombea Urais Ecuador auawa kwa kupigwa risasi

0
29

Mgombea urais katika uchaguzi ujao nchini Ecuador, Fernando Villavicencio ambaye alifanya kampeni kwa kuweka wazi uhalifu na vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya maafisa wa serikali, amepigwa risasi na kuuawa kwenye mkutano wa kampeni.

Villavicencio, mwanachama wa bunge la kitaifa la nchi hiyo ambaye awali alikuwa mwandishi wa habari, alipigwa risasi nje ya shule moja huko Quito baada ya kuzungumza na wafuasi vijana na mshukiwa mmoja kuuawa katika vurugu zilizofuatia huku watu wengine tisa wakipigwa risasi.

Kundi la uhalifu linalojulikana kama Los Lobos (The Wolves) la pili kwa ukubwa nchini humo lenye wanachama takribani 8,000, limedai kutekeleza shambulio hilo katika video iliyowaonesha wamevalia barakoa wakionesha ishara za kundi lao na kutikisa silaha zao.

Ecuador kihistoria imekuwa nchi yenye usalama na utulivu katika Amerika ya Kusini, lakini uhalifu umeongezeka katika miaka ya hivi karibuni kutokana na uwepo wa makundi ya dawa za kulevya ya Ki-Colombia na Ki-Mexico, ambayo yameingia katika makundi ya uhalifu.

Send this to a friend