Mgombea wa upinzani ashinda Urais visiwa vya Shelisheli

0
23

Mwanasiasa wa upinzani Wavel Ramkalawan ameshinda uchaguzi wa Uraid nchini humo akiwa ni mgombea wa kwanza wa upinzani kushinda wadhifa huo tungu visiwa hivyo vipate uhuru kutoka kwa Uingereza miama 40 iliyopita.

Tume ya uchaguzi imemtangaza kuwa mshindi baada ya kupata kura asilimia 54.9 dhidi ya Rais aliye madarakani, Danny Faure aliyepata asilimia 43.5.

Ramkalawan, kiongozi wa chama cha Democratic Alliamce ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la Anglican anakuwa Rais wa tano wa visiwa hivyo.

Mwanasiasa huyo amegombea nafasi hiyo kwa mara sita ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 alipitwa kwa kura 193.

Akizungumzia ushindi huo amesema kwamba uchaguzi huo haumaanishi kwamba kuna watu walioshinda na kushindwa, bali ni mifumo tu ya kuoata viongozi wa kuongoza nchi na kwamba atashirikiana na viongozi wote.

Send this to a friend