Mgonjwa apona Virusi vya UKIMWI

0
47

Wakati Virusi vya UKIMWI vikiendelea kuitikisa dunia kutokana na kutokuwa na dawa, mwanaume mmoja kutoka London nchini Uingereza amekuwa mtu wa pili duniani kupona virusi hivyo, madaktari wameeleza.

Adam Castillejo amepona ikiwa ni miezi 30 baada ya kucha kutumia Antiretroviral (ARV), dawa zinazofubaza makali ya virusi hivyo.

Matabibu wameeleza kuwa Adam hajaponeshwa kwa kutumia dawa za Virusi vya UKIMWI bali kupitia matibabu ya upandikizaji wa seli (stem-cell transpant) kwa ajili ya saratani aliyokuwa akipatiwa.

Mwaka 2011 Timothy Brown kutoka Berlin nchini Ujerumani aliripotiwa kuwa mtu wa kwanza kupona virusi hivyo, miaka mitatu na nusu baada ya kupatiwa matibabu kama hayo.

Upandikizaji wa seli unaonekana kuzuia virusi hivyo kuzaliana zaidi ndani ya mwili kwa kubadili seli za kupambana na magonjwa kwa kutumia seli za mchangiaji (donor) ambazo zinaweza kupambana na Virusi vya UKIMWI.

Send this to a friend