Mgonjwa wa nne wa VVU aripotiwa kupona

0
34

Mwanaume mmoja (jina limehifadhiwa) huko California ambaye ameishi na Virusi Vya Ukimwi tangu mwaka 1980 amepona virusi hivyo wakati akipewa matibabu ya saratani ya damu.

Mwanaume huyo alipokea huduma ya matibabu katika kituo cha tiba ya saratani cha City of Hope huko Duarte, California, ambapo taarifa kutoka kwa madaktari wake zinasema mgonjwa alifanyiwa upandikizaji wa uboho ili kuondoa chembe chembe za damu zenye saratani.

Kinana akerwa na utitiri wa trafiki barabarani

Baada ya upandikizaji, mgonjwa alifuatiliwa na kuwa chini ya uangalizi kwa zaidi ya miezi 17, na baada ya hapo viwango vya VVU havikuonekana mwilini mwake.

“Tunafuraha kukujulisha kwamba VVU yako imepungua na huhitaji tena kutumia tiba ya kurefusha maisha ambayo umekuwa ukitumia kwa zaidi ya miaka 30,” alisema Dk. Jana Dickter, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka City of Hope.

Mwanaume huyo anaripotiwa kuwa mwathirika wa nne kupona virusi hivyo huku mwathirika wa kwanza ulimwenguni akiwa Timothy Brown mwaka 2011, hata hivyo Brown alifariki kwa saratani mnamo Septemba 2020.

Send this to a friend