Mahakama ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imemhukumu aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri hiyo, Paulo Teveli kifungo cha miaka 20 jela bila faini baada ya kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa Machi 19, mwaka huu na Hakimu Hellen Hozza huku shauri hilo la uhujumu Uchumi Na 23/2022 likiendeshwa na Wakili Suzan Kimaro.
Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ambayo ni matumizi mabaya ya mamlaka chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329, na kosa la ufujaji na ubadhirifu wa shilingi 8,377,000 ambazo ni za makusanyo ya kila siku kutoka kwa wagonjwa ambazo hakuzipeleka benki katika kipindi cha mwaka 2020.
Aidha, mbali na adhabu hiyo mshtakiwa ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu ambazo ni mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same.