Miaka 20 jela kwa kukata nyaya za TTCL

0
22

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mohamed Mwichui kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na kuisababishia hasara ya shilingi milioni 5.8.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi amesema mshtakiwa amefanya kosa kukata nyaya zinazotumika kwa ajili ya mawasiliano, na mahakama imemtia hatiani baada ya kushindwa kuthibitisha kuwa nyaya za TTCL zilizokuwa nyumbani kwake alipelekewa na mtu aliyemtaja kwa jina la ‘Dokta’ wakati wa utetezi wake.

“Mahakama inakuhukumu kifungo cha miaka 20 jela ili iwe fundisho kwa wengine, na haki ya kukata rufaa ipo wazi iwapo hujaridhika na hukumu hii,” amesema Hakimu Kyaruzi.

Mkuu wa Polisi Nigeria ahukumiwa kwenda jela miezi mitatu

Awali, mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzi adhabu kwa kuwa ana familia inayomtegemea akiwemo mtoto mdogo, hata hivyo mahakama imemuamuru kulipia gharama ya shilingi milioni 5.8 kama hasara aliyoisababishia TTCL.

Send this to a friend