Miaka 30 jela kwa kumbaka mlemavu wa viungo na akili

0
58

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemhukumu kwenda jela miaka 30, Juma Ligamba (40), mkazi wa kijiji cha Kibubwa wilayani Butiama kwa kosa la kumbaka mlemavu wa viungo na akili.

Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo, Denis Bigambo amesema mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 Septemba 20 mwaka huu majira ya jioni katika kijiji cha Kibubwa wilayani humo.

Vyumba vya madarasa Sengerema vyageuzwa madanguro

Akielezea tukio hilo, amesema siku ya tukio mshtakiwa ambaye ni jirani wa mhanga alifika katika nyumba hiyo baada ya kubaini kuwa mama wa binti hakuwepo na hivyo kuingia ndani moja kwa moja alipokuwa amelalala binti huyo kisha kuanza kumbaka.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 9, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba ambapo amesema mahakama imejiridhisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo na hivyo anastahili kutumikia kifungo hcho kwa mujibu wa sheria.

Send this to a friend