Miaka 50 jela kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania

0
41

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewatia hatiani watu sita wakiwemo watatu wa familia moja na kuhukumiwa kwenda jela miaka 50 kwa kosa la kula njama kutaka kuipundua Serikali ya Tanzania.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Seif Chombo, Abdallah Chombo, Mohamed Kamala, Athumani Chombo, Omary Mbonani na Rashid Ally.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Dkt. Yose Mlyambina amesema Januari Mosi 2014 na Julai 13, 2020 kwenye maeneo tofauti wilayani Tunduru mkoani Ruvuma na maeneo mengine watu hao walikula njama ya kufanya ugaidi.

Amesema washtakiwa hao wanadaiwa kula njama kuanzisha vita ya kidini vilijulikanavyo kama Jihad na kuwashawishi vijana kuongeza nguvu kuipundua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanzisha taifa la Kiislamu kwa kutumia nguvu na machafuko.

Aidha, ameeleza kuwa washitakiwa walipelekwa nchi mbalimbali zenye uongozi wa Kiislamu kwa ajili ya mafunzo zaidi ya Jihad kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mahakama iliwapa haki yao ya msingi kama hawakubaliani na adhabu iliyotolewa wanaruhusiwa kukata rufani.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend