Miaka 7 jela kwa kumkashifu Rais Samia kupitia WhatsApp

0
32

Levinus Kidanabi maarufu kama ‘Chief Son’s amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela na faini ya TZS milioni 15 kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 19, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu, Matha Mahumbuga ambapo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.

Mchungaji kortini kwa tuhuma za kutapeli bilioni 1.6

Imeelezwa kuwa shtaka la kwanza na la pili alilotenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa la mtandao wa WhatsApp maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu huku shitaka la tatu likiwa kutumia namba ya simu isivyo kihalali bila kuwa na klibali kutoka mamlaka husika.

“Katika makosa hayo yote mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya TZS milioni 5 kwa kosa la kwanza, miaka miwili jela na faini ya TZS milioni 5 kwa kosa la pili na miaka miwili jela pamoja na faini ya TZS milioni 5 kwa kosa la tatu,” amesema Wakili wa Serikali Daniel Masambu.

Send this to a friend