Michezo yote ya Ligi Kuu Tanzania kufanyika Dar es Salaam

0
79

Kurejea kwa shughuli za michezo nchini Tanzania baada ya kusimamishwa kwa miezi miwili kutokana na janga la corona kunarejea na mabadiliko makubwa ambapo mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho zilizosalia zitachezwa Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ikiwa ni utekeleza wa tamko la Rais Dkt Magufuli ambaye ameruhusu shughuli za michezo kurejea kuanzia Juni 1, 2020.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa viwanja vitakavyotumiwa kwa michezo iliyosalia ni Uwanja wa Taifa, Uwanja wa Uhuru na Chamazi Complex.

Aidha, amesema kuwa michezo ya Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili itafanyika jijini Mwanza, na viwanja vitakavyotumika ni CCM Kirumba na Nyamagana.