Miili ya wanafunzi saba waliofariki kwa radi yaagwa, Rais Samia agharamia misiba

0
3

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kuaga miili ya wanafunzi saba wa Shule ya Sekondari Businda iliyopo wilayani Bukombe mkoani Geita waliofariki kwa kupigwa na radi mnamo tarehe 27 januari, 2025.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko ameongoza shughuli za kuaga na kukabidhi ubani kwa wafiwa huku akiwataka kuwa wavumilivu hasa kipindi hiki cha majonzi.

Aidha, amesema Rais Samia amegharamia msiba pamoja na kutoa ubani kwa kila familia za wafiwa pamoja na kugharamia usafirishaji wa miili ya wanafunzi wawili kwenda Chato, Geita na Karatu mkoani Arusha kwa mazishi.

“Rais Samia amegharamia msiba pamoja na kutoa ubani kwa kila familia za wafiwa pamoja na kugharamia usafirishaji wa miili ya wanafunzi wawili kwenda Chato, Geita na Karatu mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.

Wanafunzi hao saba waliokuwa wakisoma kidato cha tatu walikuwa na umri kati ya miaka 16 na 18, walikutwa na umauti kwa kupigwa na radi wakati wakiendelea na masomo darasani.

Waliofariki ni Erick Emmanuel Akonaay (17), Nikas Paul Tompoli (18) Gabriel Daud Makoye (17), Doto Marco Masasi (18), Asteria Reonard Mkina (16), Peter Nkinga Manyanda (17) na Erick Martine Bugalama (16).

Send this to a friend