Miili ya watu wanne yaokotwa Handeni, Tanga

0
152

Jeshi la Polisi mkoani Tanga limesema limeokota miili ya watu wanne wakiwemo wanaume watatu na mwanamke mmoja katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Handeni mkoani humo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema Julai 3, 2025 iliokota mwili wa mwanaume mmoja ambao umebainika kuwa ni wa Benard Masaka (43), mfanyabiashara wa bucha, huku chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa wivu wa kibiashara, na tayari watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema miili mingine miwili ya wanaume ambayo ilikutwa porini katika maeneo tofauti Handeni bado haijatambuliwa na kwamba inaendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Kwa upande mwingine, Jeshi la polisi limesema linawashikilia watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa jina la Fatma Athuman (24) mkazi wa Kidereko, Handeni Februari 28, 2025, na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe.

Send this to a friend