Uhalifu unaweza kumaanisha aina mbalimbali za vitendo visivyo halali au vinavyokiuka sheria katika jamii. Kuna makundi mengi ya uhalifu ambayo yanajumuisha mambo kama vile wizi, mauaji, udanganyifu, unyanyasaji wa kijinsia, na biashara haramu.
Umasikini, ukosefu wa fursa za elimu, na kutokuwepo kwa usawa wa kiuchumi huleta mazingira ambayo watu wanaweza kugeukia shughuli haramu kama njia ya kujikimu.
Baadhi ya miji barani Afrika inachukuliwa kuwa hatari sana kutokana na viwango vya uhalifu kuwa vya juu kufuatia matukio yanayohusiana na dawa za kulevya, utekaji nyara, na hata mizozo ya silaha.
Hapa ni orodha ya miji 10 barani Afrika yenye kiwango kikubwa cha uhalifu mwanzoni mwa mwaka 2024;
1 Pretoria – Afrika Kusini
2 Durban – Afrika Kusini
3 Johannesburg – Afrika Kusini
4 Port Elizabeth – Afrika Kusini
5 Cape Town – Afrika Kusini
6 Lagos – Nigeria
7 Windhoek – Namibia
8 Harare – Zimbabwe
9 Nairobi – Kenya
10 Casablanca – Morocco