Miji 5 Afrika yenye watu wenye uwezo mkubwa kifedha

0
43

Katika miji ya Kiafrika, ambapo kuna tofauti wa mapato na upatikanaji wa mahitaji unatofautiana sana, uwezo wa kununua bidhaa au huduma ni kiashiria muhimu cha ustawi wa kifedha.

Watu walio na uwezo zaidi wa kununua bidhaa au huduma, wanaweza kutimiza mahitaji yao ya kimsingi, kupata elimu bora, huduma za afya pamoja na kuweka akiba kwa ajili ya siku zijazo.

Hata hivyo, hali hii haipo kila mahali, baadhi ya miji mingi ya Afrika inakabiliwa na changamoto zinazopunguza uwezo wa wakazi kupata bidhaa na huduma kutokana na ukosefu wa ajira, ukosefu wa usawa wa mapato, na mfumuko wa bei.

Hii ni miji mitano ya Kiafrika yenye watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha kulingana na Numbeo;

  1. Pretoria – Afrika Kusini
  2. Johannesburg – Afrika Kusini
  3. Cape Town – Afrika Kusini
  4. Durban – Afrika Kusini
  5. Nairobi – Kenya
Send this to a friend