Miji 5 inayoongoza kuwa na foleni barani Afrika mwaka 2024

0
100

Barani Afrika, foleni barabarani ni tatizo kubwa linaloathiri maisha ya kila siku ya mamilioni ya watu. Nchi nyingi za Afrika zinakumbana na changamoto hii inayosababisha hasara za kiuchumi, upotevu wa muda, na kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira.

Miongoni mwa sababu zinazosababisha foleni barabarani ni ukuaji wa haraka wa miji, miundombinu duni, na ongezeko la umiliki wa magari.

Katika miji kama Lagos, Nairobi, na Cairo, ukosefu wa barabara nyingi za kuingia na kutoka huongeza msongamano wa magari. Barabara kuu za njia moja na mitaa myembamba huwa vizuizi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.

Hii ni miji mitano ya Afrika yenye kiwango cha juu cha foleni mwaka 2024 [kwa dakika];

  1. Lagos – Nigeria: 68.8
  2. Nairobi – Kenya: 52.7
  3. Cairo – Misri: 49.9
  4. Pretoria – Afrika Kusini: 45.
  5. Cape Town – Afrika Kusini:42.5
Send this to a friend