Mikoa 11 itakayokosa umeme kwa saa 12 Jumatatu

0
52

Mikoa 11 ya Tanzania itakosa  umeme kwa saa 12 Novemba 15 mwaka huu kutokana na matengenezo yanayofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa.

Umeme utakatika kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 jioni ili kupisha matengenezo yanayolenga kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.

Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha Kilimanjaro na Tanga.

TANESCO imewaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza.

Send this to a friend