Mikoa 12 yenye kiwango kikubwa cha udumavu Tanzania

0
83

Udumavu wa lishe, au utapiamlo, ni hali inayojitokeza wakati mwili wa mtu unapopata au kutumia lishe isiyo bora au duni. Sababu kuu ni upungufu wa virutubisho muhimu kama vile protini, vitamini, madini, na nishati (kalori) katika lishe yao.

Udumavu wa lishe unaweza kusababisha athari mbaya kwa afya, ikiwa ni pamoja na ukuaji mdogo, upungufu wa kinga mwilini, na hatari zaidi ya kupata magonjwa.

Katika hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika mkoani Manyara, ameeleza kuwa licha ya Serikali kuchukua hatua za kupambana na udumavu wa lishe nchini, kazi kubwa bado inahitajika ili kupunguza kiwango cha utapiamlo na kuhakikisha lishe bora inapatikana kwa wananchi.

Hii ni mikoa yenye kiwango kikubwa cha udumavu wa lishe nchini,

1. Iringa: 56.9%
2. Njombe: 50.4%
3. Rukwa: 49.8%
4. Geita: 38.6%
5. Ruvuma: 35.6%
6. Kagera: 34.3%
7. Simiyu: 33.2%
8. Tabora: 33.1%
9. Katavi: 32.2%
10. Manyara: 32%
11. Songwe: 31.9%
12. Mbeya: 31.5%

Send this to a friend