Mikoa 5 inayoongoza kwa mimba za utotoni Tanzania

0
74

Mimba za utotoni ni hali inayotokea wakati msichana mwenye umri wa chini ya miaka 18 anapata ujauzito. Hali hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya mtoto, afya yake, na mustakabali wake.

Katika hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022, amesema pamoja na Tanzania kupunguza viwango vya mimba za utotoni kutoka asilimia 27 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 22 mwaka 2022, lakini bado kuna juhudi za kuendelea kupunguza viwango hivyo ili kuwalinda watoto.

Rais Samia amesema mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Shinyanga imepunguza viwango vya mimba za utotoni kwa kasi kubwa zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine.

Mikoa 12 yenye kiwango kikubwa cha udumavu Tanzania

Aidha, amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam viwango vya mimba za utotoni vimeongezeka kutoka asilimia 11.9 hadi asilimia 18.1 na mkoa wa Njombe viwango vimepanda kutoka asilimia 19.7 hadi asilimia 25.5 huku Ruvuma ikipanda kutoka asilimia 32 hadi asilimia 37.2.

Hii ni mikoa yenye viwango vikubwa zaidi vya mimba za utotoni;
1. Songwe: 45%
2. Ruvuma: 37%
3. Katavi : 34%
4. Mara: 31%
5. Rukwa: 30%

Send this to a friend