Mirabaha: Serikali yaanda mfumo wa kutambua nyimbo zinazochezwa redioni

0
36

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema mfumo utakaokuwa ukihesabu na kutambua nyimbo zinazochezwa katika vituo vya redio unatarajiwa kukamilika Oktoba 2021, na ndiyo utaanza kufanya kazi rasmi.

”COSOTA mna kazi kubwa ya kufanya na kuhakikisha mnakusanya fedha za kutosha ili gawio la mwezi Desemba liwe lenye hamasa kwa wasanii wetu. Ni imani yangu kuwa kwa kanuni hii mpya na viwango hivi mlivyopanga kuwa vinalipika kikubwa katika hili ni kuweka mifumo ya kiteknolojia ambayo itarahisisha makusanyo hayo,”amesema Dkt. Abbasi.

Amesema hayo wakati akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Innocent Bashungwa alipoiagiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa makusanyo ya mirabaha pamoja na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa mirabaha na kuziwasilisha wizarani mwisho mwa mwezi Septemba.

Bashungwa amesisitiza kuwa anahitaji kupata makadirio ya makusanyo ya mirabaha hiyo kwa mwaka huu wa fedha na kuanzisha utaratibu ambao atakuwa akifuatilia hali ya makusanyo hayo kwa kila mwezi kwa kuhakikisha anapata taarifa.

Send this to a friend