
Miss Tanzania mwaka 2023, Tracy Nabukeera ametangaza kuwa hatoshiriki Mashindano ya Miss World 2025.
Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii, amesema uamuzi huo ni kutokana na kukosa uungwaji mkono na kutokuwa na maandalizi ya kutosha kushiriki mashindano hayo makubwa.
“Uamuzi huu haukuwa rahisi, lakini kutokana na kukosa uungwaji mkono, mawasiliano ya wazi na maandalizi ya kutosha kutoka kwa shirika linalohusika, sikujiona tena kuwa na uwezo wa kutosha kuiwakilisha Tanzania katika hatua hiyo ya kimataifa,” amesema.
Aidha, akizungumza na Clouds Fm, Mkurugenzi na Msimamizi wa Mashindano ya Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi amesema Tracy Nabukeera aliwaandikia barua ya kutoshiriki mashindano ya Miss World 2025 ili kushughulikia matatizo ya afya akili yaliyokuwa yakimsumbua, hivyo taasisi haikumtegemea Kwenda kuiwakilisha nchi.