Mitandao 5 ya kijamii inayotumika zaidi Afrika kwa mwaka 2023

0
52

Mitandao ya kijamii ni majukwaa na huduma za mtandaoni ambazo huwezesha watu kuwasiliana, kushirikiana, na kubadilishana maudhui kwa njia ya dijiti. Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kisasa, ikichangia katika mawasiliano, burudani, na biashara mtandaoni.

Mwezi wa Agosti 2023, GeoPoll ilifanya utafiti katika nchi kadhaa barani Afrika kujua ni kwa kiwango gani mitandao ya kijamii inatumiwa na kwa lengo gani. Hapa inaeleza;

Facebook
Facebook bado inaendelea kuwa mfalme asiye na mpinzani wa mitandao ya kijamii barani Afrika, ikiwa na watumiaji wanaofikia milioni 170 kote katika bara hili. Jambo la kushangaza ni uwezo wa jukwaa hilo kuvuka mipaka ya tamaduni na lugha na kuwaunganisha watu kutoka asili tofauti. Ni kweli kwamba asilimia 82 wanashiriki kikamilifu katika Facebook. Asilimia 68 hutumia Facebook kutafuta habari na matukio ya sasa, wakati asilimia 49 hutumia kujenga urafiki mpya.

TikTok
Wakati umaarufu wa TikTok umeongezeka kimataifa, kuibuka kwake kwa haraka barani Afrika kunashangaza. Kwa kiwango cha asilimia 60 cha watumiaji wanaoshiriki kikamilifu, TikTok imejikita katika nafasi ya pili miongoni mwa majukwaa ya mitandao ya kijamii katika eneo hilo. Katika mtandao huo, asilimia 73 ya washiriki hutumia TikTok kwa kutazama na kushiriki video fupi, huku asilimia 72 wanaiona kama chanzo cha kupata burudani kwa video za ucheshi. Asilimia 61 ya watumiaji hutegemea TikTok kujifunza ujuzi mpya na kugundua mbinu za maisha.

Instagram
Asilimia 54 wanashiriki Instagram kikamilifu. Hata hivyo, mshangao mkubwa ni kwamba asilimia 62 ya watumiaji hutumia Instagram kuchunguza yaliyomo katika ubunifu na asilimia 61 zaidi wanafuatilia kwa kiasi kikubwa watu maarufu na wanasiasa, wakati asilimia 59 wanashiriki kikamilifu kwa kuposti picha zao wenyewe na kuhifadhi kumbukumbu.

Vigezo vilivyozingatiwa na CAF kuchagua mwenyeji wa AFCON

X (Twitter)
Mtandao wa X (iliyokuwa Twitter awali) ilishika nafasi ya nne katika uchunguzi uliofanyika, ikiwa na asilimia 49 ya washiriki na kama chanzo cha habari. Asilimia 78 ya watumiaji kwa kiasi kikubwa hutumia X (Twitter) kufuatilia vyanzo vya habari. Zaidi ya hayo, Asilimia 59 hutumia jukwaa hilo kujenga uhusiano na watu wenye mawazo kama yao na kushiriki katika mazungumzo na mijadala yenye maana.

Reddit
Reddit inaweza kuwa na asilimia 6 tu ya watumiaji barani Afrika, lakini athari yake ni kubwa na ya kushangaza. Miongoni mwa watumiaji hawa, asilimia 75 wanajihusisha kwa kiasi kikubwa katika mazungumzo kuhusu maslahi au shughuli za binafsi na asilimia 68 ya watumiaji hutumia maudhui yenye kina na taarifa za kuelimisha. Ingawa inaweza kuwa na idadi ndogo ya watumiaji, Reddit inathibitisha kwamba ubora mara nyingine huwa na uzito zaidi kuliko wingi, na hivyo kuifanya iwe jukwaa la kufuatilia katika eneo la mitandao ya kijamii barani Afrika.

Send this to a friend