Mjema: Rais Samia aachwe afanye kazi alete maendeleo

0
36

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema amewataka vijana kukilinda chama hicho pamoja na mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan na kutokubali kuyumbishwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mjema amesema vijana wanakazi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika chama  na taifa kwa ujumla, hivyo wahitimu hao wahakikishe wanajibu hoja  pindi wanapoona chama na viongozi wanasemwa vibaya.

“Kilindeni sana Chama cha Mapinduzi  hususani Mwenyekiti wetu, tulinde chama na viongozi wake, hatuko tayari mwenyekiti wetu achezewe au kuyumbishwa, aachwe afanye kazi ya kuleta maendeleo,” amesema.

Aidha, amewataka vijana hao kutumia  vyema elimu waliyopata vyuoni kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.

Send this to a friend