Mkaguzi Mkenya akiri kuiba bilioni 1 nchini Marekani

Raia wa Kenya, Tobias Otieno (41) anakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka minne hadi 12 jela nchini Marekani, baada ya kukiri kuiba zaidi ya dola 400,000 [TZS bilioni 1] za fedha za walipa kodi alipokuwa akifanya kazi kama mkaguzi wa hesabu wa serikali katika jimbo la New York.
Otieno amekiri kutenda kosa hilo kati ya mwaka 2022 na 2024, ambapo alihamisha fedha kutoka akaunti za manispaa kwenda kwenye akaunti binafsi za biashara alizokuwa akizidhibiti.
Waendesha mashtaka wamesema Otieno aliiba dola 405,843 kutoka Mamlaka ya Mji wa Wallkill katika Kaunti ya Orange, wakati huo, alikuwa amepangiwa kazi kama mkaguzi wa serikali.
Otieno, ambaye inaripotiwa alikuwa akipata mshahara wa takribani dola 75,000 [TZS milioni 192.9] kwa mwaka katika nafasi yake, amefukuzwa kazi.







