Mkandarasi aagizwa kulipa bilioni 2 kwa kutokalimisha mradi kwa wakati

0
36

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ameagiza kampuni ya Sogea Satom kutoka nchini Ufaransa inayotekeleza mradi wa maji wa Butimba kulipa adhabu ya kisheria ya malipo ya shilingi bilioni 2.5 kutokana na kuzembea kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Mbali na kushindwa kukamilisha mradi huo kwa wakati, kampuni hiyo imedaiwa kuongeza kinyemelea muda wa mkataba kwa kufanya kazi hiyo bila kuujulisha uongozi wa mkoa ambapo awali iliahidi kumaliza mradi huo Julai 31 mwaka huu.

Makalla amedai mkandarasi huyo aliongezewa miezi mitatu mbele kinyemela ikiwa ni mara ya pili, na kudau kuwa hali hiyo haikubaliki na ni kinyume cha maagizo ya Rais Samia Suluhu aliyetaka mradi huo kukamilika kwa wakati.

“Hiki kitendo narudia kusema hakikubaliki. Ni lazima mkandarasi huyu akatwe hiyo fidia ili fedha hizo zimuume, kwani ni dhahiri hatambui wananchi wa Mwanza wanavyotaabika na kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu,” amesema Makalla.

Serikali yaagiza atakayeuza sukari kwa zaidi ya TZS 3,200 ashtakiwe

Ameongeza, “hili jambo linashangaza sana. Mkandarasi amelipwa fedha kwa asilimia 100 na niliwaahidi wananchi kuanza kupata huduma ya maji ya uhakika kuanzia Julai 31 baada ya kuongezewa muda Februari, mwaka huu. Huyu mkandarasi hana sababu yoyote ya kuongezewa muda lakini sasa lazima amalizie hiyo miezi mitatu pamoja na malipo hayo ya fedha, kwa kweli sijaridhika kabisa.”

Aidha, Makalla ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kukaa na Wizara ya Maji kuanza utekelezaji wa agizo la kumkata fedha hizo ili iwe fundisho kwa makandarasi wengine.

Send this to a friend