Mkazi wa Moshi ashitakiwa kwa kuishi kinyumba na mama na wanae wawili

0
35

Mpagazi mmoja (jina limehifadhiwa) mkazi wa Kata ya Mwika Kaskazini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anashitakiwa kwa kuishi kinyumba na mama na wanawe wawili, akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne (17), kama wake zake.

Akizungumza wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mradi wa jitihada za jamii katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto na wanawake unaoendeshwa na shirika la KWIECO, mwanaharakati, Dorcas Mringo amesema mpagazi huyo ambaye anafanya kazi ya kubeba mizigo ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro alikuwa na uhusiano wa kingono na mama mzazi wa mabinti hao na kisha mama huyo akamwozesha binti yake ambaye alikaa miaka mitatu bila kupata mtoto.

Chalamila: Walioziba vichochoro Kariakoo wabomoe kwa mikono yao wenyewe

“Baada ya binti wa kwanza kushindwa kufika kushika ujauzito, mama akamwozesha tena binti yake wa pili ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Lyakrimu,” amesema.

Ameongeza kuwa baada ya binti huyo wa kidato cha nne kukatisha masomo kutokana na ujauzito, baba yake mzazi alifuatilia kujua kwanini mwanae haendi shule, na ilipogundulika alikimbilia kutoa taarifa kwa wanaharakati hao wa haki za binadamu.

Send this to a friend