Mke ashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mume wake akishirikiana na hawara

0
44

Jeshi la Polisi Mkoani Songwe linamshikilia mke na hawara yake kwa tuhuma za mauaji ya mumewe, Victor Mwakapenda (41) mkazi wa Mtaa wa Ilembo wilayani Mbozi huku chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa marehemu alitoweka nyumbani tangu Aprili 30 mwaka huu wakiwa na mke wake, na baadaye mwili wake ulipatikana Mei 9, mwaka huu katika msitu wa Mpoloto uliopo Kijiji cha Igale Wilaya ya Mbeya vijijini.

Mahakama yamhukumu miaka 90 kwa ubakaji

Ameongeza kuwa baada mwili huo kukutwa kwenye msitu ulipelekwa kwenye hospitali ya Ifisi jijini Mbeya na kuhifadhiwa mpaka ndugu zake walipoutambua juzi Mei 29 mwaka huu na kukabidhiwa kwa ajili ya mazishi.

Mpaka sasa polisi wanawashikilia watu wawili wanaosadikika kuhusika na tukio hilo akiwemo mke wa marehemu na dereva pikipiki ambao hawakutajwa majina yao kwa sababu za kiuchunguzi.

Send this to a friend