Mkurugenzi asimamishwa kwa kuwaonea muhali wabadhirifu

0
39

Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Hassani Njama Hassani kwa kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya Machi 10 mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa fedha za miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine, zilizotolewa kwa ajili ya bwalo la chakula, jiko na bweni kisha.

Baada ya kubaini hayo alimuagiza mkurugenzi kuwachukulia hatua za kiutumishi wakuu wote wa idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo, lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhilifu wa fedha za umma.

Send this to a friend