Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Wakili Kiomoni Kibamba amesema hakuna wajawazito wanaojifungulia chini katika Kituo cha Afya cha Buzuruga mkaoni Mwanza, na kwamba picha zinazosambazwa mtandaoni ni za Septemba 2022.
Katika taarifa kwa umma, Kibamba ameeleza kuwa awali kituo hicho kilikuwa na vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia, na baada ya kuona kumekuwa na ongezeko la wanaojifungua, serikali iliongeza idadi ya vitanda na kufikia sita.
BoT yaonya wanaotumia pesa kutengeneza maua
“Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inapenda kuuhakikishia umma kuwa katika Kituo cha Afya cha Buzuruga, hakuna wakinamama wanaojifungulia chini kama taarifa ya mitandaoni inavyoonyesha,” imeeleza taarifa.
Sambamba na hilo, imesema Serikali imejenga jengo la mama na mtoto lenye uwezo wa kulaza wakina mama 42 lililogharimu TZS milioni 200 ambazo ni fedha za mapato ya ndani ya halmashauri, lengo likiwa ni kuondoa adha ya wakina kulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja.