Mkurugenzi Ilemela: The Cask Bar haina leseni ya kuuza chakula wala vileo

0
40

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imetangaza kuifungia baa maarufu inayojulikana kama The Cask Bar & Grill iliyoko jijini Mwanza kwa muda wa siku 30 baada ya kudaiwa kukiuka masharti ya leseni.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Halmashauri ya Ilemela imesema baada ya kufanya uchunguzi wa kina imejidhihirisha kuwa baa hiyo ilikiuka utaratibu kwa kuendesha biashara ya vileo bila leseni, kuendesha biashara ya shisha bila leseni pamoja na kuendesha biashara ya chakula bila leseni.

Wanahabari na watumishi wa Serikali washambuliwa na Morani Ngorongoro 

Akizungumza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Kiomoni Kibamba ameeleza kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya uongozi wa baa hiyo kufanya matangazo ya kibiashara kinyume na sheria ya matangazo ya vileo kifungu cha 86 ambapo sheria inakataza kuchanganya biashara za matangazo na shughuli nyingine tofauti na masharti ya leseni.

“Hapa kuna biashara mbili ya mgahawa na vileo ambazo zote hana leseni zake, kwahiyo huu siyo utaratibu wa kuendesha mambo, kwahiyo tumezuia kwa muda mpaka utaratibu ufuatwe,” amesema.

Kibamba amesema mbali na biashara hiyo kukiuka masharti ya leseni pia imebainika kutokuwa na leseni ya biashara kwa kipindi cha miaka miwili.

Send this to a friend