Mkurugenzi Uhuru Media, wasaidizi wake wasimamishwa kazi

0
46

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Media, Ernest Sungura, Mhariri Mtendaji, na Msimamizi wa Gazeti, Rashid Zahoro kumnukuu isivyo sahihi Rais Samia Suluhu Hassan.

Uamuzi huo umetangazwa leo na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongo baada ya gazeti hilo kupotosha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hana mpango wa kugombea urais mwaka 2025.

Mbali na hilo, Chongolo amesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku saba.

Send this to a friend