Mkurugenzi wa kampuni ya JATU amwandikia barua DPP kukiri makosa yake

0
57

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (33) anayekabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kujipatia fedha kiasi cha TZS bilioni 5.1 kwa njia ya udanganyifu, amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kukiri mashitaka yake na kuomba kupunguziwa adhabu.

Mshitakiwa huyo ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Richard Kabate wakati kesi hiyo ilipotajwa.

Kupitia wakili wake, Nafikile Mwamboma amesema mshitakiwa ameandika barua kwa DPP tangu Aprili 20, mwaka huu akiomba kukiri mashitaka yake ili aweze kuimaliza kesi hiyo.

Mkurugenzi huyo anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika SACCOS ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo cha mazao ili kuzalisha faida zaidi, wakati akifahamu fika kuwa si kweli.

Send this to a friend