Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Mahera atumiwa barua ya vitisho

0
37

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Charles Mahera amesema licha ya mafanikio makubwa ambayo taasisi hiyo inajivunia anapitia kipindi kigumu kwani amepokea barua ya vitisho kutoka nje ya nchi kuhusu masuala ya uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mahera amesema amepokea barua hiyo kutoka kwa raia wa Marekani anayefahamikama kwa jina la Robert Amsterdam akiitisha NEC.

“Kwa hiyo kama Taifa mjue ni majaribu tuliyonayo ambayo haya majaribu lazima muendelee kuyaombea,” amesema Mahera.

Aidha, amekemea vitendo vya baadhi ya watu ksema kuwa fulani atakwenda The Hague (Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu) na amewataka kutumia muda huo kueneza sera na si vitisho.

Kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, NEC imesema kuwa tayari yamekamilika kwa asilimia 80. Taasisi hiyo imewaonya wananchi kutokuuza vitambulisho vya kupigia kura, badala yake wavitunze ili watimize haki yao ya msingi.

Send this to a friend