Mkuu wa Jeshi la Sudan amfukuza kazi kamanda wa jeshi la akiba

0
44

Mkuu wa Jeshi la Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amemfuta kazi makamu wake ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti.

Jenerali Burhan na Hemedti wamehudumu kama mwenyekiti na naibu wake wa Baraza la Uongozi, mtawalia, tangu mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 2021.

Baada ya uamuzi huo wa Jenerali Burhan kumfuta kazi Hemedti badala yake amemteua aliyekuwa kiongozi wa waasi ambaye pia ni mjumbe wa Baraza Kuu, Malik Agar kuwa naibu wake.

Burhan ameiagiza sekretarieti ya Baraza Uongozi na mamlaka husika za serikali kutekeleza agizo hilo mara moja.

Mwezi uliopita mkuu huyo wa jeshi alilivunja jeshi la akiba na kutangaza kuwa wapiganaji wake ni waasi baada ya mvutano wa kimadaraka kuibuka kati ya marafiki hao wa zamani.

Tangu wakati huo nchi hiyo imeingia kwenye mapigano yaliyopeleka vifo na watu kukimbia makazi yao pamoja na kuathiri uchumi wa Taifa hilo.

Send this to a friend