Mkuu wa Jeshi Sudan afungia akaunti za benki za jeshi la akiba (RSF)

0
47

Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametoa agizo la kuzifungia akaunti zote za benki za jeshi la akiba (Rapid Support Forces) pamoja na kampuni tanzu zake zote.

Amri hiyo, imetolewa Jumapili, Mei 14 ambapo bado haijulikani ni athari zipi zitakazojitokeza kwa RSF na jinsi maagizo ya Burhan yatakavyotekelezwa.

Jenerali Burhan pia amewastaafisha maafisa wanne wa kijeshi wanaohusishwa na kundi hilo akiwemo Brigedia Jenerali Omar Hamdan Ahmed, kamanda wa RSF Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, na ambaye kwa sasa anaongoza ujumbe wa jeshi la wanamgambo kwa mazungumzo ya amani na jeshi la Sudan huko Jeddah, Saudi Arabia.

Mwanasiasa afungwa kwa njama za kuiba figo

Jenerali Burhan pia amemfuta kazi Gavana wa Benki Kuu, Hussain Yahia Jankol na kumteua Borai El Siddiq badala yake. Mpaka sasa hajatangaza sababu za kumfuta kazi Jankol.

Tangu katikati ya Aprili, Jeshi la Sudan na RSF chini ya Burhan na Dagalo ambao wanaoongoza nchi hiyo, wamekuwa kwenye mvutano wa kuwania madaraka ambao umewalazimu maelfu kukimbilia nchi jirani.

Send this to a friend