Mkuu wa Mkoa ataka wasioimba wimbo wa Taifa watozwe faini TZS 10,000

0
56

Baada ya kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule kuiomba Serikali kuwatoza faini angalau TZS 10,000 kwa wale wote ambao hawatoimba wimbo wa Taifa au wasiouimba vizuri, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamesema uzalendo haujengwi kwa kulazimishwa.

Rosemary alitoa kauli hiyo katika maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ambayo iliibua mjadala katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa hilo ni suala la uzalendo linalotoka moyoni.

Zitto: Wanasiasa jivueni minyororo ya mwaka 2020

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Paul Loisulie amesema uzalendo haujengwi kwa kulazimishwa bali kwa kuelimishwa na kuonyeshwa uzuri.

“Kuna namna tunaweza kufanya zaidi ya kutoza faini, hasa kufundisha shuleni ili wanafunzi wakiwa watoto wanafahamu kuimba wimbo wa Taifa. Hilo ni muhimu kuliko hili la kulazimisha. Kwa kutoza faini hili halitaenda, tujikite shuleni uzalendo utajijenga wenyewe,”amesema.

Aidha, Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Deus Kibamba amesema suala hilo linahusu mmomonyoko wa maadili na kutoheshimu tunu za Taifa.

“Ukishaona watu wanaona bendera inashshwa wao wanapita ujue kuna shida hapo. Kama ameshindwa kuheshimu bendera ataheshimu vipi fedha za maji zilizotumwa wizarani? amehoji.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend