Mkuu wa Polisi Nigeria ahukumiwa kwenda jela miezi mitatu

0
47

Mahakama Kuu nchini Nigeria imemhukumu Mkuu wa Polisi nchini humo, IGP Usman Alkali Baba kifungo cha miezi mitatu jela kwa madai ya kutotii amri ya mahakama.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Mobolaji Olajuwon bin kufuatia kesi ya Afisa mmoja wa zamani wa polisi, Patrick Okoli anayedai kuwa amestaafu kinyume cha sheria na kwa lazima kutoka katika Jeshi la Polisi la Nigeria.

IGP Usman ametakiwa kutumikia kifungo cha miezi mitatu jela au kutii amri ya mahakama ya kumrejesha kazini ofisa huyo wa polisi iliyotolewa tangu Oktoba, 2011.

Apple yatishia kuiondoa Twitter kwenye App Store

Mahakama hiyo pia imeamuru malipo ya N10million (TZS milioni 52.9) kwa mwombaji kama fidia maalum kwa kunyimwa haki na marupurupu kinyume cha sheria na kinyume cha katiba kama Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi la Nigeria kuanzia 1993 hadi sasa.

Send this to a friend