Mkuu wa UDSM, Dkt. Jakaya Kikwete akagua Hosteli za Magufuli zilizotumika kama karantini

0
10

Vyuo vikiendelea na michakato ya kuanza tena masomo Juni Mosi mwaka huu, hatua mbalimbali zimechukuliwa na vyuo husika pamoja na serikali kuhakikisha kuwa wananfunzi wanakuwa salama.

Katika hilo, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ametembelea Hosteli za Magufuli zilizokuwa zikitumika kama karantini kwa wagonjwa wa corona, ili kujiridhisha endapo ni salama kwa wanafunzi kuzitumia.

Akiwa katika hosteli hizo, serikali imemuhakikishia kuwa imechukua hatua zote za muhimu, na kwamba hosteli hizo zipo tayari kutumiwa tena na wanafunzi.

“Leo nikasemaa waliochukua hosteli hizi watangaze rasmi wao wenyewe kwamba wameshafanya yote waliyoahidi ya kuzitayarisha kuwa salama, kwahiyo tunashukuru kwa kauli ya kwamba pako salama,” amesema Dkt. Kikwete.

Hivi karibuni Rais Dkt. Magufuli alitangaza uamuzi wa kufungua vyuo vyote pamoja na kuanza masomo kwa wanafunzi wa kidato cha sita kuanzia Juni Mosi mwaka huu, kufuatia kupungua kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Send this to a friend