Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Afrika Kusini ashitakiwa kwa ufisadi

0
104

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Afrika Kusini, Luteni Jenerali Dumisani Khumalo amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za udanganyifu na ufisadi.

Kwa mujibu wa vyombo vya Habari vya Afrika Kusini, Khumalo alikamatwa Alhamisi jioni baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Johannesburg na kikosi cha kupambana na rushwa.

Jenerali Khumalo na maafisa sita wa juu wa polisi wanahusishwa na matumizi mabaya ya fedha za ujasusi na uteuzi wa maafisa wa polisi unaodaiwa kuwa kinyume cha sheria.

Kukamatwa kwa maafisa hao kumeibua maswali mengi kuhusu uadilifu wa kitengo hicho, ambacho kinategemewa kuzuia uhalifu na kukabiliana na wahalifu.

Send this to a friend