Mlemavu wa ngozi akatwa mkono na kufariki mkoani Mwanza

0
63

Watu wasiojulikana wamemkata mkono wa kulia na kumsababishia kifo Joseph Mathias (50) mwenye ulemavu wa ngozi, katika kijiji cha Ngulla mkoani Mwanza usiku wa Novemba 02, 2022.

Kupeleka tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha wanawakamata watu wote waliofanya ukatili huo.

Malima amewahakikishia famila hiyo kuwa Serikali itahakikisha watuhumiwa waliofanya tukio hilo wanasakwa na kukamatwa popote walipo na watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mbu wa bara la Asia ahamia barani Afrika

“Hili jambo ni baya sana na limetutia doa hivyo naliagiza Jeshi la Polisi na vyombo vingine ndani ya wiki moja wanieleze ni kitu gani kilitokea hapa maana wanaoamini kwamba unaweza kutengemeza maisha kwa viungo vya watu wengine naamini walishakwisha ila leo imenidhihirishia kwamba bado mambo haya yapo kwenye jamii,” amesema.

Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa, Mairi Makori amesema Mathias alikuwa amelala nyumbani kwake kwenye kijiji cha Ngulla ambapo aliitwa na mtu aliyefika nyumbami hapo na kugonga mlango huku akimwita jina afungue mlango na alipotoka nje alishambuliwa na kukatwa mkono wa kulia.

Send this to a friend