Mlinzi awafungia wanafunzi 17 kwenye kontena baada ya kuchuma embe changa

0
73

Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia mlinzi aliyefahamika kwa jina moja la Yusuph (27) kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa tuhuma ya kuwafungia ndani ya kontena wanafunzi 17 wa shule ya Msingi Muungano kwa madai ya kuchuma embe changa kwenye eneo lake la lindo karibu na shule hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Juma Suleiman amesema mtuhumiwa huyo aliwafungia wanafunzi hao kwa zaidi ya saa tatu kwenye kontena hilo na kupelekea watoto hao kuwa dhaifu kwa kukosa hewa.

“Bahati nzuri tulipata taarifa kupitia mkaguzi wa Kata hiyo na baadaye tukaweza kuwaokoa. Tumewaokoa katika hali ambayo wameshaanza kutokwa jasho kwa wingi na wengine miili yao ilianza kuwa dhaifu kwa kukosa hewa,” amesema Kamanda.

Amuua mkewe kisa kapika nyama ya mbuzi wakati hakuacha pesa ya matumizi

Aidha, Kamanda Suleiman amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Send this to a friend