Upasuaji wa kurekebisha ‘shape’ Mlongazila kuanza Oktoba 27

0
42

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imetangaza kuanza zoezi la upasuaji wa kibingwa kwa ajili ya kupunguza uzito na upasuaji shirikishi (Cosmetic Surgery na Bariatric Surgery).

Daktari Bingwa wa Upasuaji, Erick Mumba amesema ni mara ya kwanza nchini kufanya upasuaji huo unataotarajia kufanyika kuanzia Oktoba 27 mwaka huu hospitalini hapo hivyo kutoa wito kwa Watanzania wenye uhitaji kutumia fursa hiyo.

“Huduma hii ya kupunguza uzito kwa hapa Hospitali ya Muhimbili- Mlongazila gharama yake itakuwa ni nafuu sana ukifananisha na watu walivyokuwa wakienda kuitafuta huduma hii nje ya nchi,” amesema.

Huduma hiyo itahusisha kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu za mwili kama vile kuongeza matiti na sehemu za nje, kupunguza mafuta tumboni, na kuondoa nyama iliyozidi mwilini.

Send this to a friend