Mmiliki wa shule achukua vitu vya ndani vya wazazi walioshindwa kulipa ada

0
77

Mmiliki wa shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Green Pasture, Julius Mathew, anadaiwa kukamata samani za wazazi wanaodaiwa ada ya watoto wao kama fidia katika shule.

Kitendo hicho kimelalamikiwa na wazazi na kuiomba Serikali kuingilia kati hali hiyo kwa madai kuwa ni udhalilishaji unaofanywa na mmiliki wa shule hiyo iliyoko wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Mmoja wa wazazi hao, Nembrisi Mollel mkazi wa Sekei anadai alifikia hatua hiyo kwa madai kuwa ni amri ya mahakama ili kufidia deni lake la TZS 630,000 ya ada ya mtoto wake aliyekuwa akisoma katika shule hiyo, kati ya mwaka juzi na mwaka jana.

“Ninachoshangaa ni kufuatwa na polisi wenye silaa, wakitaka kuchukua vyombo vya ndani bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kuonana na uongozi wa kijiji au balozi,” amesema.

Akizungumza kuhusu tuhuma hizo, mmiliki wa shule hiyo amesema uongozi uliamua kuwapeleka mahakamani wazazi 18 walioshindwa kulipia ada watoto wao shule ya msingi na wengine kumaliza masomo na kuondoka, hivyo uongozi unadai zaidi ya TZS milioni 14 za malimbukizi hivyo mahakama iliamuru akamate mazao ikiwemo vyombo lakini alikosa msaada wa viongozi wa kijiji.

Send this to a friend