Mmoja wa Watanzania wawili waliopotea nchini Israel afariki dunia

0
35

Mmoja wa vijana wawili wa Kitanzania wanaoaminika kushikiliwa mateka na kundi la Hamas tangu kuanza kwa mapigano na Israel Oktoba 7 mwaka huu, Clemence Felix Mtenga amefariki dunia.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeeleza kuwa marehemu Clemence alikuwa ni miongoni mwa vijana wa Kitanzania wapatao 260 waliokwenda nchini Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo chini ya Mpango wa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Rais wa Malawi azuia yeye na baraza la mawaziri kusafiri nje

“Tayari Wizara imechukua hatua stahiki ikiwemo kuijulisha familia na inaendelea kuwasiliana na Serikali ya Israel kuhakikisha kwamba taratibu za kuurejesha mwili wa marehemu nchini kwa ajili ya mazishi zinakamilika kwa wakati,” imeeleza taarifa.

Aidha, Wizara imeeleza kuwa inaendelea kufuatilia taarifa za Mtanzania mwingine, Joshua Mollel ambaye bado hajulikani alipo pamoja kuwasiliana na mamlaka za Israel kuhakikisha Watanzania wote waliopo nchini humo wanakuwa salama wakati wote.

Send this to a friend