Mnada wa kuuza vitu vya Mandela nchini Marekani umesitishwa

0
16

Mnada wa kuuza vitu binafsi takribani 70 vya Hayati Nelson Mandela ikiwa ni pamoja na vifaa vyake vya kusikia, fimbo na miwani ya kusomea umesitishwa huko New York nchini Marekani.

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti haikueleza sababu za kuhairishwa kwa mnada huo ulipangwa kufanyika Februari 22, 2023 lakini wengi wamehusisha na malalamiko yaliyotolewa na Afrika Kusini.

Binti mkubwa wa Mandela, Makaziwe Mandela alikuwa na mpango wa kuuza vitu hivyo kwenye mnada huo, akisema angependa kutumia pesa hizo kujenga bustani ya kumbukumbu karibu na mahali alipozikwa.

Afrika Kusini yapinga vitu vya Hayati Mandela kupigwa mnada Marekani

Shirika la Mali ya Urithi la Afrika Kusini (Sahra) lilipinga uamuzi wake mahakamani, lakini ilishidwa kesi hiyo na kuahidi kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Mjukuu wa Mandela, Ndaba, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema yeye pia anapinga mnada huo akisema kuwa kuuza vitu vya Mandela ni kuiibia Afrika Kusini urithi wake.

Send this to a friend