Mnyika: CHADEMA subirini ahadi ya Rais Samia

0
38

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wanachama wake kuendelea kusubiri ahadi ya Rais Samia ya kukamilishwa mchakato wa kuruhusiwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika wakati akifunga mafunzo ya mawakala wa usajili wa wanachama wa chama hicho jimbo la Morogoro Mjini katika mfumo wa kidigitali ikiwa ni moja ya mikakati ya kuimarisha chama.

Jeshi la Polisi lakanusha madai ya CHADEMA

Mnyima amebainisha kuwa Septemba 15 mwaka huu, Rais Samia alitoa ahadi kuwa haitachukua muda mrefu vyama vya siasa kuendesha mikutano yao ya hadhara.

“Kikao cha Baraza Kuu la CHADEMA kilitoa muda maalumu wa kusubiri ahadi ya Rais juu ya uendeshaji mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa aliyoitoa Septemba 15, hivyo tuendelee kuvuta subira,” amesema.

Send this to a friend