Mobeto: Rick Ross ni rafiki yangu, tunafanya biashara

0
108

Hamisa Mobetto amekana madai kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Rick Ross.

Mrembo huyo kutoka Tanzania amesema kwamba rapa huyo ni rafiki yake na kwamba uhusiano wao ni kibiashara na sio kimapenzi kama ambavyo baadhi ya watu wanadai.

“Sisi ni kama familia kubwa na tumefanya vitu pamoja ambavyo nitavizindua hivi karibuni,’’ amesema.

Ameeleza hayo katika mahojiano na runinga ya NTV nchini Kenya, na kusisitiza zaidi kwamba kwa sasa anajikita kutengeneza chapa yake ili kuweza kufanya biashara zaidi.

Tetesi za wawili hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi zilishika kasi mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya picha na video zao kusambaa wakila bata Dubai.

Send this to a friend