MOI: Hatuwakati miguu bodaboda kwa makusudi

0
41

Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo (MOI), Prof. Abel Makubi amekanusha dhana iliyojengeka juu ya bodaboda kukatwa miguu wanapofikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma ambapo amefafanua kuwa hatua ya kuondoa kiungo kwa mtu aliyepata ajali ama kwa sababu za magonjwa, hufanywa ili kuzuia madhara yasisambae zaidi mwilini.

“Wanaolazimika kukatwa miguu ni wale ambao wamepata matatizo ambayo akiendelea kukaa na mguu utasababisha madhara makubwa kwenye sehemu nyingine ya mwili, mwingine unakuta mguu umeoza ukiendelea kukaa na ule mguu itabidi sasa ukate mguu wote, hakuna mtu anayependa kukata kiungo cha mtu iwe mkono au mguu,” amesema.

JKCI kuja na tiba ya upungufu wa nguvu za kiume

Aidha, amewataka wagonjwa wanaowekewa vyuma mwilini kuhakikisha wanabadili vyuma hivyo kwa wakati ili kuepuka kujirudia kwa tatizo kutokana na chuma kutokufanya kazi ipasavyo.

Send this to a friend