MOI yalaani kitendo cha mgonjwa ‘kubusiana’ wodini

0
44

Menejiment ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imelaani kitendo cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na mgonjwa (jina limehifadhiwa) ambaye alifanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) Julai 9, mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa MOI,  na kwamba mgonjwa huyo amekiri kufanya kitendo hicho ambacho ni kinyume cha maadili ya Kitanzania.

“Tukio hilo liligunduliwa na muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho, na menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika,” imesema taarifa ya MOI.

Aidha, imesema uchunguzi umebaini wakati tukio hilo likifanyika kuna mgonjwa mwingine jirani ambaye alikuwa akirekodi video na kuituma kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unaozuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa ikiwemo kurekodi video wodini.

Imeongeza kuwa inaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo ili kujiridhisha kuwa hakukuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa wagonjwa wakati ndugu wanawatembelea wagonjwa wodini.

Send this to a friend